21 Februari 2013 - 20:30

Watu 16 wamekufa na wengine 208 kujeruhiwa baada ya mtu mmoja kujilipua akiwa ndani ya gari iliyokuwa na mabomu katika makutano ya barabara iliyo karibu na makao makuu ya chama tawala cha al-Baathi mjini Damascus, Syria.

ABNA ilinakili kutoka CRI- Shuhuda wa tukio hilo ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, mlipuko huo umetokea katika makutano ya msikiti wa al-Eman na makao makuu ya chama cha Baath katika wilaya ya al-Mazraa inayopakana na barabara ya al-Thawra. Baada ya mlipuko huo, polisi walifanikiwa kumkamata mtu mwingine aliyekuwa akiendesha gari iliyotegwa mabomu katika eneo hilo.